Leteipa the King
Página inicial > L > Leteipa the King > Ndoto ya mchana

Ndoto ya mchana

Leteipa the King

Teipas tales


Iyeeh iyeeh iyeeh
Ni vampk
lalalalalala lalalalalaa

Niliskia tufununu
Kwamba ulipata mwingine
Anayekupenda zaidi ya mimi
mtafunga ndoa pengine
Yetu ilikuwa shadow
mapenzi yenu yamekolea
Lazima huwa Anakupa
vitu sikuwa nakupea
Ndoto zako zote
ulizoniambia
Naona kama kweli sasa zinatimia
Na Sina chochote
cha kukuambia
Ila nakonda Kweli nikikufikiria

Sura yako umbo lako jamani eeh
Busu na mahaba chumbani maami
Mawaidha yako nikiwa matatani eeh
Nikikumbuka najiona hayawani maami

Nawatakia mema
(Nawatakia mema)
nawatakia mema
(Nawatakia mema)
Nawatakia mema
(Nawatakia mema)
Basi kwaheri kwaheri
kwaheri Mama
(Ndoto yangu ya Mchana)

Ingawa inaniuma
niko na furaha moyoni
Kuona kwamba umepata
vyote ulivyokuwa unatamani
Naomba nipate mwaliko
wa harusi nije Nile wali
Nipige picha na wadau
nikupe zawadi kama zamani
Alafu ntapeform
kama beshte yako
kale kawimbo nilikuimbia shambani
Na nitakuinform
tunza mume wako
Japo kuna vitu zenye ninatamani

Sura yako umbo lako jamani eeh
Busu na mahaba chumbani maami
Mawaidha yako nikiwa matatani eeh
Nikikumbuka najiona hayawani maami

Ingawa ningependa
ungekuwa wangu pekee
(Nawatakia mema)
Ingawa moyoni
umeniachia kidonda
(Nawatakia mema)
Namwomba Mungu
anipatie
mwingine Kama wewe
(Nawatakia mema)
Hivo kwaheri kwaheri
kwaheri kwaheri mama
(Ndoto yangu ya Mchana)
Lakini ninaomba
unifanyie favour Moja
(Nawatakia mema)
Ukijifungua
kama ni wa kiume
mpe jina laangu
(Nawatakia mema)
Na kama ni wa kike
mpe jina la mama yangu
(Nawatakia mema)
Basi kwaherii
(Ndoto yangu ya Mchana)

lalalala lalalala
iyeeh

Letra enviada por

Encontrou algum erro na letra? Por favor, envie uma correção >

Compartilhe
esta música

Ouça estações relacionadas a Leteipa the King no Vagalume.FM

ESTAÇÕES